Tue. Nov 4th, 2025

Yanga SC imetoa toleo la pili la jezi zao za msimu baada ya jezi zote za toleo la kwanza kuisha, Yanga imewapiga chenga ya mwili wauza jezi feki ambao wameingiza jezi fake za msimu wa 2025/2026.

Yanga SC wameamua kutoa toleo la pili lenye utofauti kidogo ili kuweka utofauti maana jezi zao zimeisha ila kuna idadi ya jezi feki nyingi mtaani ambazo zimeingizwa nchini.

Utofauti wa jezi ya toleo la pili na la kwanza ni toleo la kwanza upande wa kulia kifuani una nembo ya GSM na toleo la pili upande wa kulia kifuani una nembo ya NIA.

Jezi Mpya Yanga Toleo la Pili
Jezi Mpya Yanga Toleo la Pili