Tue. Nov 4th, 2025

“Tumepokea maombi mengi kutoka kwa mashabiki wa Simba wakiomba kuchangia faini hiyo ya shilingi milioni 212 kwasa sababu wanasema kosa hilo ni lao.

Na uongozi wa Simba umeridhia kabisa maombi hayo ya mashabiki na tutaweka namba za kuchangia kwenye mitandao yetu ya kijamii na kama yupo anayetaka kulipa faini yote ya shilingi milioni 200 kwa pamoja pia milango iko wazi”

“Kampeni hii ya uchangiaji tumeipa jina la LETU SOTE, yaani hili ni letu sote.

Hivyo ile hela kama ambayo ulipanga kuiweka kwa ajili ya kiingilio sasa hivi unaweza kuituma kwenye lipa namba tutakazotangaza ili kumaliza deni hili la CAF.”- Ahmed Ally, Afisa Habari Simba SC.