Baba Mzazi wa Mchezaji Kibu Denis Afariki Dunia

Mchezaji wa Simba Sc, Kibu Denis amefiwa na bab yake mzazi, Msee Denis Prosper usiku wa kuamkia leo huko Mkoani Kigoma.

Uongozi wa klabu ya Simba SC umetuma salamu za rambirambi kwa mchezaji wao Kupitia taarifa rasmi iliyotolewa na klabu hiyo, Simba imeeleza masikitiko yake makubwa kwa msiba huo mzito, ikimfariji Kibu pamoja na familia nzima ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.

Simba imetoa wito kwa Wanasimba na wadau wote wa michezo nchini kuwa pamoja na Kibu kwa sala na maombi, ili aweze kupata nguvu na utulivu wa kurejea katika majukumu yake ya soka baada ya msiba huo.
Marehemu Mzee Prosper anatajwa kuwa alikuwa mtu wa karibu na mwanae, na kifo chake kimeleta huzuni kubwa ndani ya familia pamoja na mashabiki wa Simba Sc.

Related Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *