December 19, 2025

Magori Afunguka “Yanga Hawana Pesa ya Kumnunua Eli Mpanzu”

0
1766143682525.jpg


Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya klabu ya Simba Sc Crescentius Magori amefunguka mambo mazito kuhusiana na tetesi zinazoeleza kwamba winga hatari wa klabu hiyo Ellie Mpanzu anaweza kujiunga na Yanga Sc katika dirisha dogo la usajili ambalo litafunguliwa mwezi Januari 2026.

Crescentius Magori katika taarifa yake aliyoitoa siku ya leo Ijumaa December 19 akiwa anafanya mahojiano na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam ameeleza wazi kwamba tetesi za Mpanzu kwenda kujiunga na Yanga Sc mwezi Januari ni habari za uongo na zinapaswa kupuuzwa mara moja.

Magori katika taarifa yake hajataka kupepesa macho bali ameeleza wazi kwamba hapa Tanzania hakuna klabu yoyote yenye uwezo wa kununua mkataba wa Ellie Mpanzu kwani ni mkataba ambao unagharimu pesa nyingi sana tofauti na inavyoelezwa na vyanzo mbalimbali vya habari za michezo nchini Tanzania.

Magori katika taarifa yake amerusha dongo zito kwa watani zao wa jadi yaani Yanga Sc ambao wanahusishwa na tetesi za kuhitaji saini ya Mpanzu ambapo amewaeleza wazi kwamba viongozi wao hawana pesa ya kumng’oa Ellie Mpanzu katika klabu ya Simba Sc kutokana na vipengele vilivyopo kwenye mkataba wake wa sasa.

Magori amewataka viongozi wa klabu ya Yanga Sc waachane na tabia za kuwaongopea mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kwa kuwaeleza kwamba watainasa saini ya Mpanzu mwezi Januari kwani hawana ubavu wa kufanya hivyo kutokana na bajeti ya timu yao.

Magori amewataka mashabiki na wanachama wa klabu ya Simba Sc waachane na tabia ya kusikiliza na kuamini sana propaganda za mitandaoni bali kwa wakati huu wajikite zaidi kufuatilia maendeleo ya klabu yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *