Huyu Hapa Kocha Mpya wa Simba

Simba SC imemtangaza Steven Barker Raia wa Afrika Kusini kuwa Kocha wao mpya, Steven Barker (57) alikuwa Kocha wa Stellenbosch ya Afrika Kusini toka 2017.
Steven Barker amewahi kufundisha timu za University of Pretoria (2008-2014) na Amazulu (2014-2016) na amewahi kuzichezea timu Wits University (1990-1998) na SuperSport United 1999-2000.
Barker hajawahi kucheza wala kufanya kazi nje ya Afrika Kusini, je anaweza kuisaidia Simba SC kama alivyofanikiwa kuifanya Stellenbosch kuwa timu nzuri yenye soka safi?
