Aziz Ki Afunguka Kuhusu Ahoua, Anatakiwa Kujengwa Kisaikolojia

AZIZ KI KUHUSU AHOUA?
“Mimi namuamini Ahoua, nadhani anaweza kurudia kiwango chake bora, itategemea yeye mwenyewe anataka nini, kitu ambacho watu wanatakiwa kuelewa msimu uliopita ametumia nguvu kubwa sana, amecheza mechi nyingi na kuisaidia timu yake kwa kiasi kikubwa.
“Labda msimu huu ameanza kwa kukabiliana na uchovu, inawezekana aliamini akifanya vizuri anaweza kupata nafasi nyingine mbali lakini akajikuta bado yuko hapa, kwa hiyo anatakiwa kujengwa kisaikolojia, hiyo ni kawaida kumtokea mchezaji yeyote
