Wed. Nov 5th, 2025
CLement Mzize

Mshambuliaji wa Yanga Clement Mzize ataendelea Kubaki yanga licha ya kuhusishwa Kujiunga na Timu mbalimbali Nje ya Tanzania.

Taarifa Kutoka makao Makuu ya Klabu zimedokeza Kwamba Uongozi umefanikiwa kumshawishi Mzize kwa Kumpa Mkataba Mpya utakaomfanya Kusalia Jangwani Hadi Mwaka 2028.

ALSO READ | Ahmed Ally: Jezi Zetu Hazina Shida Sio Mbaya, Mimi Nimezipenda Sana

Awali Mzize alikuwa na Mkataba wa Miaka Miwili,Lakini kwasasa ameongezewa Mwaka mmoja zaidi,Pamoja na Kupewa nyongeza ya Mshahara na Gari Jipya.

Klabu ya Esperance de Tunis ya Tunisia iliripotiwa kuwasilisha Ofa ya Dola Milioni 1 kwa ajili ya Kumnasa Mzize hata Hivyo Yanga iliweka Ngumu kumuuza na Kuweka Kipaumbele cha Kumshawishi Mzize abaki Yanga.

Kila kitu Kimekamilika Tayari na Mzize Ataendelea kuwatumikia yanga Hadi Mwaka 2028.

ALSO READ | ORODHA ya Vilabu Bora Afrika 2025 (CAF Club Ranking)