
“Tumeziona jezi ambazo zimevujishwa usiku wa Jana zikisemekana ndo jezi zetu za msimu huu, sijajua lengo kubwa la waliovujisha ni nini!?, Huenda ni kutaka KUHARIBU Biashara ya Jayrutty.
“Yote ya yote, binafsi Nimezipenda sana zile jezi, kutokana na upekee ulizokuwa nazo kulinganisha na jezi za misimu ya awali, ambazo kuna muda tunazindua jezi tukawa tunajiuliza “Hii sinkama ya Msimu flani”.
Maua yaliyopo kwenye Ile Jersey ni ya KIPEKEE sana na nimeyapenda mnoooooo.!
“Shida inakuja, mtu aloyovujisha ana roho ngumu sana, ameàmua kutumia sijui simu ya wapi, picha ni za hivyo sana..mbaya zaidi akaona atandike kwenye Baraza na kuelekea Bafuni, ule sio uungwana hata kidogo, Sijaenda”
ALSO READ | Jezi Mpya za Simba Zilizovuja Mtandaoni Zazua Gumzo