Ligi Kuu Tanzania Bara inarejea, ratiba hii hapa JKT Tanzania vs Simba SC

Burudani ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora inarejea wikiendi hii. Sababu kubwa ya ligi kusitishwa kwa muda ilikuwa ni changamoto za kiuendeshaji zilizotokana na sababu za kiusalama na miongozo yake ni kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB), Novemba 4.
Tayari TPLB wametangaza kurejea kwa ligi hivyo wikiendi hii kazi inanedelea kwa wababe kuwa uwanjani.
Novemba 8,2025
Pamba Jiji FC vs Singida Black Stars, mchezo huu unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
JKT Tanzania vs Simba SC, mchezo huu unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mej.Jen.Isamuhyo.
Novemba 9,2025
Yanga SC vs KMC FC, Uwanja wa KMC Complex.
Namungo FC vs Azam FC, Uwanja wa Majaliwa.


Related Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *