Mzize atakuwa nje ya uwanja kwa miezi miwili akijiuguza Operesheni yake ya goti. Lugha rahisi ni kwamba Mzize ataikosa Michuano ya AFCON pale Morocco siku kadhaa mbele. Ni taarifa mbaya kwake kama mchezaji. Ni taarifa mbaya mbaya kwetu Watanzania kama Taifa. Mzize yuko njiani katika nyakati hizi. Ndiye mshambuliaji hatari kwa washambuliaji wa ndani. Anakufunga kwa kichwa. Anakufunga kwa mguu wa kulia. Anakufunga kwa kushoto. Anakufunga kwa Curve. Kiufupi kwa washambuliaji wa viwango vyetu, Mzize amekamilika. Hana tone la shaka. Kama kuna moja ya wachezaji tuliokuwa tunajisemea wanaenda kutupa kiburi cha kusema TUTAFANYA LOLOTE huko Morocco, basi ni pamoja na huyu Mzize. Majeraha yake ni taarifa mbaya sana. Ukiachana na Taifa kuathirika, lakini Yanga SC nao ni waathirika wengine wa majeraha yake. Watamkosa katika mechi mbili za kwanza kabla ya kupisha AFCON, lakini pia hatujui akirudi kiwanjani atakuwaje. Sio wachezaji wote wanaotoka katika chumba cha matibabu hapo hapo wakawasha moto. Wengi wanatumia muda mrefu kidogo kuwa sawasawa. Ugua pole teka la Ball.
