Tue. Nov 4th, 2025

KLABU ya JKT Tanzania imeweka wazi hatma ya kocha wao, Ahmad Ally, kufuatia tetesi na maswali mengi yaliyoibuka mitandaoni kuhusu Kocha huyo kuhitajika na Klabu ya Simba SC.

Kupitia taarifa yao kwa umma, JKT Tanzania imesisitiza kuwa:

  • Kocha Ahmad Ally bado ana mkataba mrefu na klabu hiyo.
  • Ana malengo ya kuyatimiza akiwa JKT Tanzania na bado yuko sehemu sahihi kwa maendeleo ya kazi yake.
  • Ana misimamo thabiti na hawezi kuyumba wala kushawishiwa na lolote nje ya klabu.
  • Wachezaji wa JKT wanategemea malezi yake kufanikisha malengo yao na hayuko tayari kuwaacha.
  • Amekabidhiwa jukumu na mwajiri wake ambalo ameapa kulitimizia mwisho.

Aidha, taarifa hiyo imeeleza kuwa kocha huyo anapenda kufanya kazi kwa uhuru na utulivu bila presha, na kwa sasa hana sababu ya kuondoka kwani anaona fursa kubwa zaidi akiwa JKT Tanzania.

JKT Tanzania imehitimisha kwa kusisitiza kuwa Ahmad Ally ni Mtanzania mzalendo, mwenye uwezo na uzoefu mkubwa, hivyo ni vyema akaachwa aendelee kutimiza majukumu yake kwa amani na utulivu ndani ya kikosi hicho.