
Anaandika @kelvinrabson_
✍️ Nafikiri kabla ya kuangalia ubora na madhaifu kwenye mchezo huu , changamoto kubwa ilikuwa ni pitch mpira hautulii na ilipelekea kukosa ubora kwa timu zote mbili .
A) TUKIANZA NA YANGA
1: Wakati wanafanya build up walitumia mipira mirefu kama silaha yao kufika eneo la juu “Long balls” kwa kutumia eneo la pembeni dhumuni ni kuwafanya Mbeya City wazuie eneo kubwa la uwanja ili nafasi ipatikane eneo la ndani .
2: Nafikiri Plan yao haikufanikiwa kwasababu walikuwa na idadi ndogo ya wachezaji kwenye box la Mbeya City ngumu kwao ( kuna nyakati Boyeli Vs wachezaji wanne wa Mbeya City ) alihitaji msaada kushinda mipira hiyo .
3: Yanga walihitaji “Special Player” mtu ambaye atafanya vitu vitokee kwa urahisi … walimkosa mchezaji kama huyo + Mbeya City walikuwa bora kwenye kuzuia ( COMPACT ) .
B) TUMALIZIE NA MBEYA CITY
1: Nimependa plan ya kocha wa Mbeya City “Malale Hamsini” waliweka ugumu kwa Yanga kushambulia nafasi kupitia katikati na wachezaji wake walikuwa active kiwanjani + Yanga hawakuwalazimisha kuwafungua ni kama walicheza kwenye mikakati yao .
2: Mbeya City walichagua vita yao ya kulinda vizuri box lao na kuwafanya Yanga kukosa nafasi kupitia kwenye kiungo na wakipora mpira wanashambulia haraka sana kwa kunufaika na kasi ya wachezaji wao wa mbele .
NOTE :
1: Kama kuna juhudi na upambanaji ambao Malale alikuwa anataka kwa vijana wake basi kaupata leo . Kila mmoja wao alikuwa yupo tayari kupambana bila hata kucheza faulo zisizo na ulazima ( ni ngumu kutaja mchezaji mmoja mmoja maana wote wamekuwa na mchezo mzuri )
2: Yani kwa ule uwanja aina ile ya football ndio ilikuwa ile pekee . Mipira mirefu , shinda mpira wa pili , mipira iliyokufa basi tena . Piga pasi ufedheheshwe
3: Diarra ameona kama alama 3 hawapati basi hata moja isikosekane … Jioniiiiiii kaonesha umahiri wake
4: Nafikiri kwa balance nzima ya mchezo hayo ni matokeo ambayo kila mtu anastahili kupata leo
FT: Mbeya City 0-0 Yanga SC
Kijana wangu bhana @kelvinrabson_ ameweza kuchambua hii mechi .! 😀