
Beki wa kushoto wa Young Africans SC (Yanga), Chadrack Boka, ameweka wazi msimamo wake kuhusu nafasi yake ndani ya kikosi cha mabingwa hao wa Tanzania Bara.
Akizungumza hivi karibuni, Boka amesema kuwa hajajiandaa kukaa benchi na kuharibu kiwango chake cha soka, hasa baada ya klabu hiyo kumsajili tena beki mwingine wa kushoto, Mohamed Hussein “Tshabalala” (35).
“Mimi ni mchezaji mwenye malengo makubwa, siko tayari kukaa benchi na kuua kipaji changu. Najua ushindani ni mkubwa, lakini nitapambana kuhakikisha nafasi yangu haipotei,” alisema Boka.
Ujio wa Mohamed Hussein, ambaye ni miongoni mwa mabeki