NGAO YA JAMII 2025 🏆

🟢 YANGA SC 🆚 SIMBA SC 🔴
⏰ 17:00
🏟️ Benjamin Mkapa.

SIKU ambayo mashabiki wa soka walikuwa wakiisubiri kwa hamu hatimaye imefika. Tunakwenda kushuhudia mchezo wa Dabi ya Kariakoo ukiwa ni ufunguzi wa msimu wa 2025-2026

Simba na Yanga katika fainali ya Ngao ya Jamii zimekutana mara tisa huku rekodi zikionyesha Simba imeshinda mechi tano na Yanga ikishinda nne. Yanga inaingia katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kuifunga Simba katika mechi tano mfululizo za mashindano tofauti walizokutana hivi karibuni.
.
Wakati Yanga ikitamba na hilo, Simba yenyewe ndiyo kinara wa kubeba Ngao ya Jamii ikifanya hivyo mara 10, ikifuatiwa na Yanga iliyochukua mara nane.