Wed. Nov 5th, 2025
Ahmed Ally Afunguka: Ni Wakati Sahihi Kwa Mohamed Hussein Kuondoka Simba
Ahmed Ally

Zikisalia siku chake kabla ya kufanyika kwa Tamasha la Simba Day linalotarajiwa kufanyika Septemba 10, 2025 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, uongozi wa Simba umeendelea kujiweka karibu na jamii kwa kutembelea na kula chakula cha pamoja na watoto yatima katika kituo cha ‘Umra Orphanage Center’ kilichopo Magomeni Mikumi jijini humo.

‎Akizungumza mara baada ya tukio hilo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa timu hiyo, Ahmed Ally, amesema hatua hiyo ni sehemu ya kuthamini na kushirikiana na jamii inayoizunguka kla-bu, huku akisisitiza ndani ya jamii hiyo pia wapo mashabiki wa Simba wanaoendelea kuipa nguvu timu hiyo.

‎“Tumekuja hapa kwa malengo mawili, kwanza ni kujiweka karibu na jamii inayotuzunguka, am-bapo tunaamini ndani yake kuna mashabiki wa Simba. Kwa kufanya hivi tunawafurahisha zaidi mashabiki wetu, hasa wenye uhitaji. Lengo la pili ni kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu kwa kuwalisha yatima, hata kama ni mara moja kwa siku. Hakuna dogo mbele za Mwenyezi Mungu, kwani malipo yake ni ulinzi na baraka kwa timu yetu ya Simba,” amesema Ahmed.

‎Aidha, ameongeza mafanikio ya klabu hiyo hayawezi kupatikana bila msaada wa Mungu kutoka-na na ukubwa wa changamoto na ushindani uliopo katika soka la Tanzania na Afrika kwa ujumla.

‎“Vita ni kubwa na upinzani ni mkali, hatuwezi kupenya bila msaada wa Mwenyezi Mungu. Ili upate msaada, lazima na wewe pia utafute radhi na baraka zake,” amesisitiza.

‎Tamasha la Simba Day linatarajiwa kushirikisha burudani mbalimbali na kuhitimishwa kwa mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Gor Mahia ya Kenya, huku mashabiki wakihamasishwa kujitokeza kwa wingi kuisapoti timu yao.