Wed. Nov 5th, 2025
Shaffih Dauda: Hakuna Beki wa Kulia Tanzania Mkali Kama Shomari Kapombe
Shaffih Dauda: Hakuna Beki wa Kulia Tanzania Mkali Kama Shomari Kapombe

Nimepata kuwashuhudia walinzi wengi wa kulia wakicheza soka kwenye ardhi hii ya Tanzania hapa nazungumzia wazawa na hata waliokuja wakitokea nje ya Tanzania

Lakini hayupo mlinzi wa kulia mwenye mwendelezo wa kiwango cha juu mechi baada ya mechi kumzidi Shomy , bado pia hayupo beki wa kulia hatari kwenye box la wapinzani kumzidi Kapombe

Kufunga sio jambo geni kabisa kwake , amefunga sana ligi ya ndani , amefunga pia kimataifa akiwa na klabu na bado anafunga Timu ya Taifa

Ukiwa na Shomari unapata uhakika eneo la ulinzi , unakuwa na matumaini ya kushuhudia assist muda wowote kutoka kwake na inapobidi basi anaimaliza mechi mwenyewe kama ilivyotokea hii leo