Taifa Stars imevuna Sh55 milioni baada ya kushinda mchezo wa pili wa fainali za CHAN 2024 kwa kuichapa Mauritania kwa bao 1-0.
Stars imechukua Sh10 milioni kutoka kwa Rais Samia Suluhu ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Goli la Mama katika michuano hiyo ambapo zilikabidhiwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila pia ametoa Sh20 milioni.
Aidha mdau wa michezo, Azim Dewji naye ameiahidi Sh25 milioni kwa timu hiyo.
Katika hatua ya makundi mashindano ya CHAN 2024, Taifa Stars inaongoza Kundi B ikiwa na pointi sita, ikishinda mechi mbili na kufunga mabao matatu.
