Tue. Nov 4th, 2025

Clement Mzize amecheza misimu miwili (2) akiwasumbua wachezaji wa kigeni ambao ndiyo ulikuwa uti wa mgongo wa Yanga.

Tangu ameingia kwenye kikosi cha wakubwa September 13,2022 akitoka kunolewa na Said Maulid chini ya Mkurugenzi wa Yanga enzi hizo Mwinyi Zahera kwenye timu ya vijana.

Mzize alikutana na moto wa Fiston Mayele aliyefunga magoli 33, msimu huo Mzize alifunga mabao matano (5) na pasi moja (1) ya goli ligi kuu pekee.

Msimu uliofuata alimlazimisha Mayale wagawane magoli Mayele akifunga 17 yeye alifunga mara 6 akitoa pasi 7 za magoli ukumbuke nyakati zote Nabi alikuwa nyuma yake.

Kuonyesha kuwa hakubahatisha hata nyakati ambazo Miguel Gamondi alipoteza uaminifu mfano msimu pita ambao Stephen Aziz Ki alionekana kuwa ndiye mshambuliaji namba moja licha ya uwepo wa Musonda, Guede ila Mzize alicheza na kufunga.

Kwenye nyakati zote wamekuja washambuliaji kama Hafiz Konkon, Joseph Guede, Prince Dube n.k lakini Mzize amefanikiwa kujiuza kimataifa na sasa anahitajika na vilabu vikubwa

Najiuliza kwenye huu msimu wanatajwa wachezaji wa kigeni pekee kuwa ni bora ila Clement Mzize simsikii licha ya kuwa na mchango mkubwa kwenye timu ni tunachagua wachezaji wa kuwasifia ama ?

England linaweza kuwa ni taifa lenye wachezaji wa kawaida lakini vyombo vya habari vikamtengeneza mcheza bora juu ya mchezaji wa kawaida

Niliwahi kumsikia mchezaji wa Ireland, James McClean, akisema kuwa Declan Rice anapokea sifa “irrelevant” kutoka vyombo vya habari vya Uingereza, akionyesha kuwa haitoshi kulalamika juu ya uwezo wake:

“the praise for Rice is excessive… He lacks the qualities of a world‑class player, such as dictating the game like Toni Kroos or Rodri.”

Mwanamichezo maarufu Gary Lineker aliweka wazi kwamba vyombo vya habari hushambulia wachezaji kwa kiwango kinachoonekana kufikia “kuharibu morali yao” kabla ya mashindano, akisema:

“It’s unique to this country to attempt to destroy our players’ morale before a major tournament. It’s weird, unpatriotic and sad.”

Kama hakuna mchezaji mzawa aliyeweza kuwa na consistency ya Mzize kwenye hii misimu minne mfululizo ukimuondoa Feisal kwa nini hatuwezi kulizungumza jina lake?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *