Homa ya Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeanza kupamba moto wakati leo ikiwa siku ya mwisho ya kuchukua na kurejesha fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi wa Shirikisho hilo.
Taarifa kutoka ndani ya kamati ya uchaguzi zinasema tayari Rais anayetetea nafasi yake Wallace Karia ametangulia kurudisha fomu hizo jana.
Karia anatetea nafasi hiyo ya Urais akiwa ameshatangulia kuongoza vipindi viwili kwenye kuliongoza Shirikisho hilo.
Leo mgombea mwingine ambaye amerudisha fomu ni Dk. Mshindo Msolla, ambaye fomu zake zimeletwa na mwanaye Mshindo Msolla.
Akizungumza mara baada ya kurudisha fomu hizo Msolla amesema tayari baba yake ameshakamilisha kujaza fomu hizo tayari kwa kuwania nafasi hiyo.
“Nimekuja kurudisha fomu za Mzee (Mshindo Msolla) Mimi ni mwanaye, na yupo tayari kwa mchakato huu,”amesema Msolla.
Akizungumzia kuhusu uidhinishwaji Msolla amesema: “Dokta Msolla ni mwanamichezo mbobevu wa mambo ya michezo kila kitu kipo sawasawa kwake na kama mnavyoona amerudisha fomu.”
Mchakato wa Uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF unaendelea, ambapo mpaka sasa wagombea wawili wa nafasi ya Rais wamerudisha fomu zao
Taarifa kutoka ndani ya kamati ya uchaguzi zinasema tayari Rais anayetetea nafasi yake Wallace Karia ametangulia kurudisha fomu hizo jana.
Karia anatetea nafasi hiyo ya Urais akiwa ameshatangulia kuongoza vipindi viwili kwenye kuliongoza Shirikisho hilo.
Ikumbukwe kuwa jana Mdau wa soka ambaye pia amewahi kuwa kwenye kamati tendaji ya timu ya Yanga Eng. Mustapha Himba amejitokeza kuchukua fomu ya Kugombea Urais wa shirikisho la soka nchini TFF huku akilalamika kukosa uungwaji mkono wa vyama vya soka vya mikoa kama katiba na taratibu za uchaguzi huo zinavyotaka