Wed. Nov 5th, 2025

Raisi wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania (TFF) Ndugu. Wallace Karia huenda akasalia kama mgombea pekee katika kinyanganyiro cha nafasi ya Urais katika Shirikisho hilo la mpira wa miguu nchini.

Hii ni baada ya Karia kukusanya Endorsement zote 47 kutoka kwa wajumbe ambao Wana haki kamili ya kushiriki uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo, hali inayopelekea kuwa mgomba pekee wa kiti Cha uraisi wa shirikisho hilo kwa mara nyingine.

Wagombea wengine wawili wamekosa Endorsement ya kuwafanya wakidhi vigezo vya kugombea uraisi huo.

Mpaka kufikia hapa Wallace Karia atagombea peke yake kwenye uchunguzi huo na kutokana na kuwa pekeyake basi itakua amepita bila kupingwa.

Wagombea wengine ambao walijitokeza kushindana na Wallance Karia walikua Ali Mayai pamoja na Mshindo Msola.

Msola ambae aliwahikuwa Mwenyekiti wa Yanga SC, alijitosa rasmi kwenye kinyang’anyiro cha Urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Fomu yake imewasilishwa kwa niaba yake na mwanawe, akionesha kuungwa mkono na familia na wafuasi wake.

Dkt. Msolla tayari alipata klabu tano zinazomdhamini, akikidhi masharti yote ya awali. Akiwa kiongozi anayeheshimika na mtaalamu wa soka, hatua yake inazidi kuleta mvuto kwenye uchaguzi huu muhimu.

Je, unadhani Karia ndiye suluhisho la kuleta mabadiliko kwenye mpira wa miguu Tanzania?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *