Tue. Nov 4th, 2025

Pappy Tshishimbi : Naichukia Sana Simba Walinifanyia Figisu Nikatemwa Yanga

Kiungo wa zamani wa Yanga Pappy Kabamba Tshishimbi ameonekana kujuta na kukiri kuwakosea watu waliomuamini wakati anatua Tanzania Yanga

“Ile mechi ya kwanza kabisa dhidi ya Simba kwenye Ngao ya jamii, ni mechi iliyo badilisha maisha yangu kwa ujumla.
Ni mechi niliyo piga kazi kweli kweli licha ya kwamba tulipoteza kwa mikwaju ya penalti. Nakumbuka baada dakika tisini mashabiki waliimba sana jina langu wengine wakinipa hela. Nikajiuliza ni upendo wa namna gani huu.
Kesho yake asubuhi tajiri mmoja hivi akanipigia simu akanipa gari mpya yenye thamani kama milioni sitini . Katika maisha yangu tangu nikiwa Mbabane sijawahi kumiliki gari ila cha ajabu siku moja tu ikawa imenipa gari

Ligi zilivyoendelea niligeuka star wa timu kiwango changu kiliwavutia Simba wakaja kuhitaji huduma yangu Isitoshe kipindi kile Yanga walikuwa na ukata kwahiyo mishahara ilikua inasusua Muda mwingine licha ya ongozi.

Bila kufikiria nikakubali kujiunga nao. Uongozi mpya ulio
ingia ukanishi nisiondoke, wanaunda project mpya Kwahiyo Kila kitu kitakuwa sawa. Rais wa timu yao akanipa mkataba ingawa sikusaini nilikuwa natembea nao. Kila alipo nipigia
simu kuuliza kuhusu mkataba nilimjibu bado kuna vipengele navipitia kwahiyo nitasaini tu alipiga simu zaidi ya
mara sita kuulizia suala la mimi kusaini ila jibu likawa ni hilo hilo tu.

Nilifanya vile nikisubiria mkataba watakao nipa Simba nione kama utakuwa na vipengele vizuri zaidi. Cha ajabu kabla siku mbili dirisha la usajili kufungwa viongozi wa SIMBA wakawa hawapokei simu zangu, nilipo rudi kumpigia Injinia Hersi alipokea akaniuliza we nani? Nilishtuka Sana lla nikamjibu mimi ni Tshimbi. Akaniuliza ulikuwa unataka nini? Daah hapo nikaamini tayari narudi Congo nikiwa nimepoteza thamani yangu. Nilidondosha machozi kiukweli, naichukia sana Simba imeniharibia maisha yangu.