
Mgombea Ubunge wa Arusha Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda, amekiri kulishwa sumu mwaka 2024 hali iliyomsababishia kulazwa Hospitalini na kutoonekana hadharani ambapo amesema kama isingekuwa Rais Samia Suluhu Hassan kusimamia matibabu yake huenda angekuwa ameshafariki.
Makonda amefichua siri hiyo leo Jumapili, September 21, 2025, wakati wa Ibada katika Kanisa la Mbingu Duniani lililopo Njiro, Arusha, akisema si mara yake ya kwanza kulishwa sumu na kwamba amenusurika kifo mara kadhaa.
“Kuna kipindi nilipotea nikaanza kutafutwa, na wengine mlinitafuta kwa nguvu kubwa huyu yuko wapi, ukweli nilikuwa naumwa, nililishwa sumu, yasingekuwa maombi ya Watanzania na Mungu kumuinua Rais Samia Suluhu Hassan kusimamia matibabu yangu nilitakiwe nife mwaka jana”