Klabu ya Benfica ya Ureno imefikia makubaliano ya kumteua mkufunzi José Mourinho kuwa kocha mkuu klabuni hapo kuchukua mikoba ya Bruno Lage aliyetupiwa virago kufuatia kipigo cha 3-2 dhidi ya Qarabag kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya siku ya Jumanne.

Meneja huyo wa zamani wa FC Porto, Chelsea, Real Madrid, Inter Milan, Manchester United na Tottenham Hotspur amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili utakaombakisha klabuni hapo mpaka Juni 2027.

Mourinho (63) raia wa Ureno ambaye pia amewahi kuinoa klabu ya AS Roma kabla ya kufanya kazi Fenerbahce na kutimuliwa mnamo Agosti 29, 2025 anarejea Benfica mahali alipoanzia kazi yake ya ukocha mwaka 2000 kabla ya kuondoka baada ya mgogoro na rais wa Benfica wakati huo.