HANS RAFAEL anasema kuwa “Kuna muda nashindwa kuelewa Wachezaji wa Yanga wanakula nini?”
“Msimu huu wamecheza mechi zaidi ya 50 kwenye mashindano yote ila ukitazama kasi, utashi, Concentration, pressing na intensity yao inatisha sana unaweza kuhisi ni mwanzo wa msimu,Yanga wako fit sana”
“Kwa kifupi leo Singida walistahili kupigwa goli 9+ kama Yanga wangekuwa na ufanisi mbele ya lango.”
“Kuna ule msemo kwamba Singida ni tawi la Yanga ila kwa huu mpira wa Yanga nani anaweza kumfunga paka kengele?, Msimu huu Yanga wamezifunga timu zote za NBC na CRDB….siyo Simba wala Azam na Singida wote wameonja joto la Yanga”
“Ni sahihi kusema Yanga ni kipimo cha mpira wa Tanzania kwa sasa” amesema Hans Rafael
.