Tue. Nov 4th, 2025

“Tunaendelea na maandalizi, tulicheza mchezo wa kwanza ndio lakini matokeo sio kitu muhimu, jambo zuri ni tunaendelea kuimarika kama timu, tukishapata muunganiko tutakuwa hatari zaidi na watu wasubiri majibu zaidi msimu ukianza kupitia miguu yangu uwanjani,”

“Nafurahi niliingia na kufunga, kwangu mimi ni kitu ambacho hakinifanyi nijishangae kwa kuwa ni kazi yangu, kitu muhimu zaidi ni kuona tuna timu nzuri, hapa kuna viungo bora na hata mabeki wenye viwango.
“Simba ni timu kubwa inataka matokeo, unaona hata kocha falsafa zake zinataka kutafuta ushindi muda wote, hili ni jambo zuri linaifanya timu kutakiwa kucheza muda wote.”