Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jacobs Mwambegele amesema August 28 hadi October 27, 2025 kitakuwa kipindi cha kampeni za Urais, Wabunge na Madiwani kwa Tanzania Bara na Zanzibar na Jumatano October 29, 2025 ndio itakuwa siku ya kupiga kura.
Akitangaza ratiba ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 wa Rais, Wabunge na Madiwani leo July 26, 2025 katika viunga vya Makao Makuu ya Tume hiyo Jijini Dodoma, Jaji Mwambegele amesema August 9 hadi August 27, 2025 itakuwa ni kipindi cha kutoa fomu za uteuzi wa Wagombea wa kiti cha Rais na Makamu wa Rais.
“August 14 hadi August 27, 2025 itakuwa ni kipindi mahususi cha utoaji wa fomu za uteuzi wa Wagombea Ubunge na Udiwani, August 27, 2025 itakuwa siku ya uteuzi wa Wagombea wa kiti cha Rais, Makamu wa Rais, Ubunge na Udiwani.
