Taarifa ya Klabu ya Yanga SC ya siku ya Jumatatu baada ya kupokea majibu kutoka CAS.
“Uongozi wa Young Africans Sports Club unapenda kuutaarifu Umma kuwa umepokea majibu kutoka Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) kuhusu kesi yetu namba CAS 2025/A/11298. CAS imeielekeza Young Africans Sports Club kurudi kwanza kwenye Kamati za ndani za Soka ili kushughulikia kesi yetu kabla ya kurudi kwao kwa ajili ya hatua za rufaa. Lakini kutokana na uonevu, uvunjwaji mkubwa wa kanuni na upendeleo wa dhahiri kwa baadhi ya timu unaoendelea kufanywa na Mamlaka za soka Tanzania, Viongozi wa Young Africans Sports Club hauna imani na hauko tayari kupeleka shauri hilo kwenye mamlaka ambazo zinatenda dhulma.
“Aidha, Vingozi wa Young Africans Sports Club unapenda kuujulisha umma kuwa, msimamo wa klabu yetu juu ya mchezo namba 184 wa Ligi Kuu msimu huu uko palepale kuwa hatutashiriki kwenye mchezo huo kwa namna yoyote ile. Wanayanga wote, watakuwa tayari kuipambania haki yao kivyovyote vile ili kukomesha dhulma na uvunjwaji mkubwa wa kikanuni unaoendelea kufanywa na mamlaka za soka kwa maslahi mapana ya maendeleo ya soka nchini”