February 5, 2026

Vilabu 10 Bora vyenye Wafuasi Wengi Facebook (Afrika)

0
1770214494513.jpg


Al Ahly Yaendelea Kutawala Afrika: Simba na Yanga Zaing’arisha Afrika Mashariki Kidijitali

CAIRO, MISRI Katika ulimwengu wa sasa ambapo soka halichezwi uwanjani pekee bali pia kwenye viganja vya mashabiki, klabu ya Al Ahly ya nchini Misri imeendelea kudhihirisha kwanini wao ni Wafalme wa Afrika kwa kuongoza orodha ya vilabu vyenye ushawishi mkubwa zaidi kwenye mtandao wa Facebook.

Utafiti wa hivi karibuni wa takwimu za kidijitali unaonyesha kuwa vilabu vya soka barani Afrika sasa vinatumia majukwaa ya kijamii kama kipimo cha umaarufu na thamani ya chapa zao (brand value) kimataifa.

Al Ahly imeketi kileleni ikiwa na wafuasi milioni 19, idadi ambayo ni zaidi ya mara mbili ya mpinzani wake wa karibu, Zamalek, inayoshika nafasi ya pili ikiwa na wafuasi milioni 8.1. Mafanikio haya ya Al Ahly yanatajwa kuchangiwa na historia yao ndefu ya mataji na uwekezaji mkubwa katika maudhui ya kidijitali Morocco na Afrika Kusini zimeonekana kutawala sehemu kubwa ya kumi bora:

Morocco: Raja Casablanca (milioni 6.4) na Wydad Casablanca (milioni 3.9) zimeendelea kuonyesha umwamba wa ukanda wa Kaskazini.

Afrika Kusini: Miamba ya Soweto, Kaizer Chiefs na Orlando Pirates, inashika nafasi ya nne na tano huku Mamelodi Sundowns ikichomoza katika nafasi ya nane.

Kwa mara ya kwanza, ushawishi wa soka la Afrika Mashariki umeanza kutetemesha majukwaa ya kimataifa. Miamba ya soka nchini Tanzania, Simba SC na Young Africans (Yanga), imefanikiwa kuingia katika kumi bora ya bara zima:

Simba SC: Inashika nafasi ya 9 ikiwa na wafuasi milioni 2.8.

Young Africans: Inafunga orodha hiyo katika nafasi ya 10 ikiwa na wafuasi milioni 2.3.

Uwepo wa klabu hizi mbili ni kielelezo tosha kuwa soka la Tanzania linakua kwa kasi na mashabiki wake wameamka kidijitali alisema mchambuzi mmoja wa masuala ya michezo.

Vilabu 10 Bora vyenye Wafuasi Wengi Facebook (Afrika)

Al Ahly Misri Milioni 19

Zamalek Misri Milioni 8.1

Raja Casablanca Morocco Milioni 6.4

Kaizer Chiefs Afrika Kusini Milioni 5.5

Orlando Pirates Afrika Kusini Milioni 5

Wydad Casablanca Morocco Milioni 3.9

Pyramids FC Misri Milioni 3.3

Simba SC Tanzania Milioni 2.8

Young Africans Tanzania Milioni 2.3

Takwimu hizi ni ishara kuwa vilabu vya Afrika sasa vimegeuka kuwa chapa za biashara zinazoweza kuvutia wadhamini wa kimataifa kupitia nguvu ya mashabiki mtandaoni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *