Viingilio Simba vs RS Berkane 25 May 2025

Viingilio Simba vs RS Berkane 25 May 2025
Viingilio Simba vs RS Berkane 25 May 2025

Viingilio Simba vs RS Berkane 25 May 2025

Klabu ya Simba imetangaza viingilio vya Mchezo wa Pili wa Fainali kombe la Shirikisho (CAF CC) dhidi ya RS Berkane utakaopigwa Jumapili ya May 25 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Jijini Dar Es Salaam.

Meneja wa Habari na Mawaailiano wa Klabu hiyo, Ahmed Ali amesema Kuwa Fainali hii itakuwa ya kipekee kuliko Fainali yoyote iliyowahi kuchezwa hapa Tanzania, ndio maana maandalizi yake yameanza mapema

Ahmed amewataka mashabiki kuchangamkia tiketi zao mapema ili kuhakikisha wanakuwa sehemu ya mashuhuda katika tukio hilo la kihistoria.

“Kuelekea katika mchezo wa hapa nyumbani, kwanza tunataka fainali yetu iwe yenye hadhi kubwa kuliko fainali zote zilizowahi kufanyika. Tunataka fainali ya Kombe la Shirikisho iwe na mvuto wa nje zaidi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Tunapiga kelele kuhakikisha mechi yetu inakuwa na mvuto mkubwa zaidi kimasoko, inazungumzwa zaidi kutokana na matukio ambayo tutayafanya”

“Tunataka kufanya fainali yenye hadhi ya juu mno, na hayo ni mambo ambayo sisi tunayamudu. Ndugu zangu fainali ndio hatua ya juu kabisa ya mashindano. Kuelekea katika mchezo huu tunatangaza viingilio na tutakaporudi kutoka Morocco tutazindua hamasa. Napenda kuwasihi Wanasimba kununua tiketi mapema. Mwakani tutacheza tena fainali lakini haitakuwa kama hii ambayo tumeisubiri kwa miaka 30.”

“Viingilio ni;

Mzunguko: Tsh. 7,000. VIP C

VIP B Tsh. 20,000.

VIP C Tsh. 30,000.

Platnumz Tsh 250,00

Hakutakuwa na daraja VIP A sababu baadhi ya wageni wa CAF watakaa eneo hilo. Wale wanangu wa VIP A wahamie eneo la VIP B au VIP C.”

“Tunazungumza na wenzetu wa N-Card kuweka wauza tiketi katika maeneo ambayo yanaonekana hayana wauzaji wengi wa tiketi. Mfano ukanda wa Tabata kuweka mtu wa tiketi. Tutasambaza mawakala wa tiketi katika kona mbalimbali za Dar es Salaam ili Wanasimba wanunue tiketi kwa urahisi.”

“Kuna watu wanatoka nje ya Tanzania kuja kuangalia fainali hii sasa Wanasimba mliopo hapa changamkieni nafasi hii. Kuepuka usumbufu Mwanasimba nunua tiketi yako mapema.”

“Kama kawaida yetu tutafanya hamasa, tunataka kufanya mchezo huu wenye hadhi kubwa na maarufu. Tarehe Mei 20, 2025 tutafanya uzinduzi wa hamasa katika viwanja vya Mbagala Zakhiem na hii itakuwa ni tofauti ya miaka yote, hii itakuwa ya kipekee. Itahusisha viongozi kadhaa wa serikali, viongozi wa Simba, wasanii mbalimbali wakubwa. Kutakuwa na matukio mengi makubwa na ya kuvutia. Kutakuwa na big screen zikionyesha mahojiano na wachezaji waliocheza fainali ya 1993 na tutaonyesha safari nzima kutoka mechi ya kwanza hadi mechi ya kuingia fainali,” alisema Ahmed

Leave a Comment

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *