Kwanza sio kweli kwamba Yanga wameshindwa kesi yao CAS, kilichoamuliwa na CAS ni kesi hii isikilizwe kwanza kwenye Kamati za ndani za Shirikisho la Mpira TFF
Kilichofanya CAS washindwe kuisikiliza kesi ya Derby ni kukosekana kwa Document ya hukumu ya Ndani ya TFF kwenye kesi ya Msingi
CAS ni Mahakama ya Rufaa na ili isikilize kesi ni lazima kuwe na maelezo yote ya kesi kwenye Mamlaka za ndani na hukumu zake zilivyokuwa
Kwanini Hakuna Hukumu ya TFF kwenye hukumu ya CAS?
Ifahamike,tukio lolote linapotokea,inatakiwa klabu husika kuwasilisha kesi yao CAS ndani ya SIKU 21
Ukichelewa hapo maana kesi inakuwa haina mashiko na CAS hawaisikilizi
Mwanzo,Yanga waliiandikia TFF kuhusu kesi yao ya Debry na kwa makusudi kabisa,TFF walikaa kimya hawakuwajibu lolote wakijua kabisa zikipita SIKU 21 Yanga watakuwa hawana pakulalamika
Hivyo Yanga wakatumia ujanja mkubwa wa kuwasilisha kwanza kesi CAS ili wawe ndani ya muda halafu wao ndio waendelee na TFF
Kesho Uongozi wa Yanga utaandika rasmi barua yao kwa TFF kama CAS walivyoelekeza na kama watakosa haki yao maana yake watakuwa na BARUA rasmi ya hukumu ya TFF itakayowasaidia CAS
HILI SAKATA BADO KABISAAA,SAKATA BADO BICHI SANA