Pazia la michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya linafungwa rasmi leo Mei 31, 2025 kwa mchezo mmoja wa fainali ambapo wanafainali wa mwaka 2020, Paris Saint-German watamenyana na Mabingwa mara tatu na wanafainali wa mwaka 2023, Inter Milan katika dimba la Allianz Arena, Munich, Ujerumani.
Inter Milan inaingia kwenye mchezo huo ikihitaji kutwaa ubingwa wa Ulaya kwa mara ya nne huku PSG ikisaka kombe hilo kwa mara ya kwanza kihistoria.
Mji wa Munich unakwenda kuandaa fainali ya klabu Bingwa Ulaya kwa mara ya tano huku PSG โikichekeleaโ siri iliyopo kwenye fainali nne zilizochezwa mjini Munich
Unaambiwa Mabingwa wote wanne waliopatikana kwenye fainali hizo walitwaa ubingwa wa Ulaya kwa mara ya kwanza, hali inayoashiria kuwa PSG atakuwa Bingwa wa UEFA 2025 kama upepo wa Munich utaendelea kuvuma kama ulivyofanya kwenye fainali zilizopita.
PSG inatarajiwa kuwa timu ya kwanza kutoka Ufaransa kutwaa ubingwa wa Ulaya tangu 1993 wakati Marseille ilipofanya hivyo ikitwaa ubingwa huo mjini Munich hali inayozidi kuchagiza ishara njema kwa PSG leo huku Luis Enrique akitarajiwa kuwa kocha wa 6 kutwaa ubingwa wa Ulaya na timu mbili tofauti kihistoria.
Inter Milan wanaingia kwenye mchezo wa leo wakitafuta kufuta ukame wa miaka 15 wa ubingwa wa Ulaya, ambapo mara ya mwisho miamba hiyo ya Italia kubeba ubingwa wa Ulaya ni mwaka 2010 wakati Jose Mourinho akiiongoza klabu hiyo kuifunga Bayern Munich 2-0 kwenye fainali katika dimba la Santiago Bernabeu.
22:00 PSG ๐ซ๐ท ๐ ๐ฎ๐น Inter Milan
๐๏ธ Allianz Arena, Munich