Nahodha wa Manchester United Bruno Fernandes atapewa muda hadi wiki ijayo kuamua kama anataka kuondoka katika klabu hiyo, huku Al Hilal wakipanga kutoa takriban £100m kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno, 30, ambaye angelipwa takriban £65m kwa msimu nchini Saudi Arabia. (Mirror)
Bayern Munich wanaweza kuanzisha mpango wa kumnunua Fernandes ingawa ada ya uhamisho ambayo United ingetaka inaweza kuwa kikwazo. (Teamtalk)4
Winga wa Argentina Alejandro Garnacho, 20, ana uwezekano mkubwa wa kuondoka Manchester United msimu huu wa kiangazi baada ya kukatishwa tamaa na majukumu yake chini ya kocha mkuu Ruben Amorim. (ESPN)
Wawakilishi wa Garnacho wanatazamiwa kufanya mazungumzo na Manchester United kujadili mustakabali wa Muargentina huyo baada ya kuenguliwa kwenye fainali ya Ligi ya Europa dhidi ya Tottenham . (Telegraph – subscription required)
Manchester United pia wanatazamia kumuuza kiungo wa kati wa Uingereza Kobbie Mainoo, 20, ili kupunguza shinikizo la kifedha kwa klabu hiyo. (Sun)
Kiungo wa kati wa Ujerumani Florian Wirtz, 22, angependelea kuhamia Liverpool badala ya Bayern Munich ikiwa ataondoka Bayer Leverkusen msimu huu wa kiangazi. (Subscription required)
Bayern Munich wanaamini kuwa winga wa Brighton na Japan Kaoru Mitoma, 28, ni mbadala wa Wirtz. (Sky Germany)
Everton wamefanya mazungumzo na mshambuliaji wa Ipswich na kikosi cha England cha vijana wenye chini ya umri wa miaka 21 Liam Delap, 22, kuhusu uhamisho wa majira ya kiangazi na pia wanavutiwa na winga wa Liverpool na Scotland Ben Doak, 19. (Guardian).
Real Madrid inamtazama kiungo wa kati wa Liverpool na Argentina Alexis Mac Allister kama mrithi wa asili wa mchezaji wa kimataifa wa Croatia Luka Modric, 39, ambaye anaondoka Bernabeu msimu huu wa joto. (Fichajes in Spanish )
RB Leipzig wamewasiliana na mkurugenzi mpya wa michezo wa Arsenal Andrea Berta kuhusu mpango unaowezekana wa kumuuza mshambuliaji wa Slovenia Benjamin Sesko, 21. (Sky Sports Germant – in Germany)
Mshambulizi wa Wolves na Brazil Matheus Cunha, 25, bado ana furaha kujiunga na Manchester United msimu huu wa kiangazi licha ya kushindwa kufuzu kwa soka la Ulaya msimu ujao. (Sky Sports)
Mlindamlango wa Aston Villa Emiliano Martinez, 32, anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo akiwa na timu za Saudi Pro League na Manchester United zinamtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina. (teamTalk)
Aston Villa , West Ham na Leeds wanatazamia kumnunua kiungo wa kati wa Southampton na Ureno chini ya umri wa miaka 21 Matheus Fernandes, 20. (Football Insider)