Simba Wakubali Yaishe, Yathibitisha Fainali Shirikisho Itachezwa Aman Complex

Simba Wakubali Yaishe, Yathibitisha Fainali Shirikisho Itachezwa Aman Complex
Simba Wakubali Yaishe, Yathibitisha Fainali Shirikisho Itachezwa Aman Complex

Simba Wakubali Yaishe, Yathibitisha Fainali Shirikisho Itachezwa Aman Complex


EditHatimaye Simba Wakubali Yaishe, Yathibitisha Fainali Shirikisho Itachezwa Aman Complex
Timu ya Simba
Timu ya Simba
Hatimaye Simba Wakubali Yaishe, Yathibitisha Fainali Shirikisho Itachezwa Aman Complex

Klabu ya Simba imethibitisha kuwa mchezo wake wa pili wa fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya RS Berkane utapigwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Simba imethibitisha hilo kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa na kuchapishwa kwenye mitandao yake rasmi ya kijamii.

Taarifa hiyo imesema

“Uongozi wa Klabu ya Simba, unapenda kuwafahamisha kuwa licha ya jitihada zote zilizofanywa na Serikali, TFF na Klabu katika kuhakikisha mchezo wetu wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya RS Berkane wa tarehe 25 Mei 2025 unafanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa zimeshindikana”.

“Kutokana na hatua hiyo mchezo huo utafanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar kama ilivyoamriwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF)”.

“Tunawaomba mashabiki na wapenzi wetu kuwa watulivu katika kipindi hiki”.

“Aidha, tutatoa taarifa rasmi za mchezo huu na hatma ya mashabiki wetu kuelekea katika mchezo huu muhimu kupitia Mkutano Maalumu na wanahabari kesho tarehe 20 Mei, 2025 saa 05:00 asubuhi katika Ofisi za Klabu ya Simba, Oysterbay jijini Dar es Salaam”.

Leave a Comment

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *