Kikosi cha Simba kimewasili jijini Arusha, ambapo kitaweka kambi ya siku moja kabla ya kuendelea na safari ya kuelekea mkoani Manyara tayari kwa mchezo wa nusu fainali Kombe la FA dhidi ya Singida Black Stars.
Mchezo huo umepangwa kuchezwa keshokutwa Jumamosi, Mei 31 kwenye uwanja wa Tanzanite Kwaraa mjini Babati.
Tayari mabingwa watetezi wa michuano hiyo Yanga wameshatangulia fainali baada ya kuifunga JKT Tanzania 2-0.