Simba SC inafahamu la kufanya ili ‘kupindua meza’

Kocha Fadlu
Kocha Fadlu

Kocha Mkuu wa Simba SC, Fadlu Davids amesema wachezaji na jopo la ufundi wanafahamu fika wanachopaswa kukifanya katika mchezo wa marejeano wa fainali ya Kombe la Shrikisho Afrika ili kubadili matokeo ya kufungwa magoli 2-0 na RS Berkane katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliofanyika Mei 17 huko Morocco.

Kocha Davids raia wa Afrika Kusini amewaambia waandishi wa habari wakati wa mkutano wa kuhusu matayarisho ya mchezo wa Jumapili Mei 25 kwamba mchezo wa kwanza Jumamosi iliyopita uliwapa mafunzo mengi ya namna ya kuwakabili Berkane nyumbani japo amekiri kuwa hautakuwa mchezo mwepesi hata kidogo.

“Berkane ni timu kubwa ina wachezaji wenye uzoefu wa kucheza fainali kuliko wachezaji wetu, lakini tutakabiliana ano vilivyo, ninaamini kila mchezaji akitekeleza majukumu yake na kujituma inawezekana kupata matokeo mazuri, Simba ni timu ambayo imakabiliana na changamoto nyingi na imekwishadhihirisha namna ya kuzikabili vilivyo na kuzishinda, tuna mashabiki wanaoiunga mkono timu yao ipasavyo” alifafanua.

Kadhalika amezungumzia kusikitishwa na mchezo huo kutofanyika kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam ambako Simba imekuwa ikipata matokeo mazuri tangu aanze kuinoa timu hiyo, yapata miezi kumi iliyopita. Lakini amesema hayo sasa yamepita na kwamba anaamini mashabiki wataendelelea kuiunga mkono timu yao hata wale ambao hawatapa fursa ya kufika uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar.

Leave a Comment

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *