Klabu ya Kengold Fc imeshuka daraja rasmi kutoka Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara kwenda Ligi ya Championship kufuatia kipigo cha 2-1 dhidi ya Wanamangush, Coastal Union katika dimba la Mkwakwani, Tanga.
FT: Coastal Union 2-1 KenGold Fc
⚽ 20’ Msimu
⚽ 37’ Bagayoko
⚽ 39’ Lipangile
KenGold Fc wenye pointi 16 wakiwa mkiani kwenye msimamo wa Ligi Kuu bara hivi sasa wamesaliwa na mechi tatu ambapo hata wakishinda zote hawawezi kuifikia Tanzania Prisons waliopo nafasi ya 14 wakiwa na pointi 27.