January 9, 2026

Pigo Kwa Aziz K, Afiwa na Mtoto wake wa Kiume

0
Aziz-Ki-Image-Yanga-SC.jpeg

Klabu ya Al-Wydad Athletic ya Morocco imetoa taarifa rasmi
ya rambirambi kufuatia kifo cha mtoto wa Mchezaji wao Aziz Ki. Kupitia
taarifa hiyo, uongozi wa klabu umeeleza huzuni kubwa na masikitiko
makubwa kutokana na msiba huo mzito.

Katika ujumbe wao, Al-Wydad wameeleza kusimama pamoja na mchezaji
huyo katika kipindi hiki kigumu, wakimuombea yeye na familia yake wapate
faraja na subira

Klabu hiyo pia imemuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu
peponi, amsamehe madhambi yake na awape familia yake nguvu, subira na utulivu wa moyo

Mwisho wa taarifa hiyo, klabu imesisitiza mshikamano wake na familia ya
marehemu, ikisisitiza kuwa msiba huo ni pigo kwa familia nzima ya
Al-Wydad.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *