Pamba Jiji Yasababisha Kagera Sugar Kushika Daraja Ligi Kuu

Kagera Sugar
Kagera Sugar

FT: KenGold 0-2 Pamba Jiji

30’, 60 Yonta Camara

Timu ya Kagera Sugar, imeshuka rasmi daraja kufuatia ushindi wa mabao 2-0 iliyopata Pamba Jiji dhidi ya KenGold FC.

Kwa ushindi huo, Pamba jiji imefikisha pointi 30 kwenye nafasi ya 11, ikifuatiwa na Tanzania Prisons nafasi ya 12 pointi 30, KMC FC nafasi ya 13 pointi 30, Fountain Gate nafasi ya 14 pointi 29 na Kagera Sugar iko nafasi ya 15 na pointi 22.

Kagera Sugar imebakiza mechi mbili ambazo hata ikishinda zote, haiwezi kufikisha pointi ilizonazo Fountain Gate.

Kagera Sugar imeungana na KenGold SC kwenye NBC Championship msimu ujao 2025/26 huku Mtibwa Sugar na Mbeya City zikirejea Ligi Kuu msimu ujao.

Leave a Comment

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *