Ndugu wa Mchezaji Victor Osimhen Wadai Kutelekezwa na Mchezaji Huyo
Familia ya mchezaji wa klabu ya Napoli ambaye anaitumikia Galatasaray kwa mkopo Victor Osimhen 🇳🇬 analalamikiwa na ndugu zake kwa kutowajali, kuwathamini na kuwatelekeza ilihali analipwa mshahara mkubwa kwenye klabu yake.
Ndugu wa Osimhen wanadai kuwa wametengwa kimaslahi na mchezaji tangu wampumzishe mama yake aliyefariki katika Jimbo la Edo, kijijini kwao. Pia wanamlalamikia kwa kutokurekebisha nyumba ya kijijini kwao ingawa anapata fedha nyingi katika kazi yake ya uanasoka.