Msimamo wa Yanga Upo Pale Pale Hawachezi, Sababu Zawekwa Wazi..Hawashawishiki

Licha ya Jitihada kubwa zinazofanywa na viongozi wa TFF na Bodi ya ligi ili kuonana na Uongozi wa klab ya Young Africans ila bado mambo yamekuwa magumu,

Msimamo wa Young Africans upo pale pale hawaitaji kuonana na kiongozi yoyote na hawautambui mchezo wa Juni 15 dhidi ya Watani zao Simba Sc,

Msimamo wa Young Africans upo:-

👉Zipi sababu za kuahirisha mchezo wa kwanza
👉Je kanuni iliamuaje baada ya Simba asc kutofika uwanjani na sio busara
👉Kwanini upangwe mchezo mwingine bila majibu ya mchezo wa awali

NAFAHAMU: Young Africans wamerejea kambini kwa ajili ya maandalizi ya michezo yao iliyosali isipokuwa dhidi ya Simba Sc,

👉Upo uwezekano wa mchezo kuchezwa ila na endapo baadhi ya Viongozi wa bodi ya ligi ambao Young Africans na vilabu vingine vinaamini wamechangia kuharibu soka la Tanzania mpska sasa watajiuzuru,

👉Pia Tff na bodi kurudi kwa Umma kuueleza ukweli na kueleza namna gani pesa za viingilio za watazamaji zitarudishwa kwa waliotoa,

👉Na Gharama walizotumia Young Africans kwenye maandalizi ya mchezo wa kwanza kurudishwa (zaidi ya milioni 50),

🙌Happ ndipo mchezo utapangiwa tarehe mpya na sio tena Juni 15.

Laa sivyo Young Africans wataendelea na ratiba zao nyingine kwakuwa wanajua na wanaamini wapo sahihi muda wote 🙌

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *