Wanachama wa Yanga ambao ni viongozi wa Matawi, wametoa msimamo mkali wakiwataka mashabiki wa timu hiyo kutobabaishwa, kwani kikosi chao hakitaenda uwanjani kwa mechi ya Dabi ya Kariakoo Juni 15, 2025.
Msimamo huo umetolewa leo na Mratibu wa Matawi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Shaaban Mgonja, aliyebainisha kuwa Baraza la Matawi limepitisha uamuzi rasmi kwamba, hawatashiriki mechi hiyo.
Mgonja ameonya kuwa, endapo Simba, Bodi ya Ligi na Waamuzi watajitokeza kwa ajili ya mchezo huo, na ikatolewa uamuzi wa Yanga kunyang’anywa pointi 15, basi kwao itakuwa mwisho wa ushiriki katika Ligi Kuu Bara msimu huu kwa kuwa hawana tena imani na uongozi wa Bodi ya Ligi.