Max Nzengeli na Pacome Zoizoua Shughuli Imeisha Jangwani

Max Nzengeli na Pacome Zoizoua Shughuli Imeisha Jangwani

Max Nzengeli na Pacome Zoizoua Shughuli Imeisha Jangwani

Kama kuna shabiki aliyekuwa akiamini Pacome Zouzoua na Maxi Nzengeli wanatimka Yanga SC kwa vile mikataba inamalizika mwisho wa msimu, basi poleni kwani mabosi wamefanya kweli kuhakikisha nyota hao wa kikosi cha kwanza wanabaki.

Pacome na Maxi waliosajiliwa msimu uliopita mikataba inaelekea ukingoni na kulikuwa na tetesi

kwamba mabosi wa Msimbazi walikuwa wakiwapigia hesabu ili kuwavuta Simba SC, jambo lililowafanya vigogo wa Jangwani kukimbizana na kila kitu kinakaaa sawa.

Mabosi wa Yanga SC wamemaliza mambo kiutu

uzima kwa kuwaita mezani na kuwaongezea miaka

miwili kila mmoja. Maxi aliyesajiliwa kutoka AS Maniema ya DR Congo na Pacome aliyetokea Asec Mimosas ya Ivory Coast walisainishwa miaka miwili walipotua Jangwani ambayo inamalizika mwisho wa msimu.

Mmoja wa viongozi wa Yanga SC ameliambia

Mwanaspoti kuwa tayari wachezaji hao wameshasaini mikataba mipya baada ya kufanya nao mazungumzo kwa muda mrefu wakishirikiana menejimenti inayowasimamia.

Mwanaspoti

Leave a Comment

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *