Kocha wa Kaizer Chiefs, Nasreddine Nabi, alikasirika alipoulizwa ikiwa bado ndiye mtu sahihi wa kuiongoza klabu hiyo kufuatia kichapo chao cha 2-1 kutoka kwa Orlando Pirates kwenye mchezo wa Soweto derby kwenye Uwanja wa FNB.
Matokeo hayo yameifanya Amakhosi kuambulia kichapo cha 12 msimu huu na wako katika hatari ya kukosa kumaliza katika nafasi ya nane bora huku wakibaki nafasi ya tisa kwenye Msimamo wa Ligi.
Nabi amekuwa kwenye shinikizo kubwa katika klabu hiyo kufuatia uchezaji wao mbaya katika Ligi Kuu ya Betway.
Alipoulizwa wakati wa mkutano wa wanahabari baada ya mechi kama anadhani bado ni mtu sahihi kwa kazi hiyo, raia huyo wa Tunisia alijibu kwa hasira na kusema ‘asichokozwe’.