Kuna muda mpira unabadilika kabisa leo sijaona ile Simba SC iliyocheza na Al Masry pale Benjamin Mkapa..Nini wangefanya ni kupeleka ule moto walioupekeka kwa Al Masry..Tatizo ikawa hakuna ile kasi na umakini na mipango thabiti mbele ya Stellenbosch FC.…Japo Mnyama kaanza kwa ushindi lakini bado kazi ipo kwani wanaenda nyumbani kwa Stellenbosch FC pale Afrika Kusini wakiwa na mtaji mdogo wa goli.
Kuna namna Simba SC wanatakiwa wawe na umakini na kufanya vitu kwa uthabiti kwani hatua hii haiitaji makosa.
FT:Simba SC 1:0 Stellenbosch FC.