Jack Diarra Aliyewafunga Simba Akiwa na Esperance Kumbe Alishataka Kusajiliwa Simba Wakamkataa
Kumbe Jack Diarra, ambaye kwa sasa anang’ara na Esperance ya Tunisia, jina lake liliwahi kupita mezani kwa viongozi wa Simba SC lakini usajili wake haukukamilika. Mchezaji huyo alionekana kwa mara ya kwanza na scout aliyewahi kufanya kazi na klabu hiyo, Mels Daalder (Double.12), alipokuwa akiichezea Burkina Faso katika michuano ya Mapinduzi Cup iliyofanyika Zanzibar. Kipaji chake kilivutia macho ya wengi, lakini kwa bahati mbaya Simba haikuweza kufikia makubaliano ya mwisho.
Wakati huo, Jack Diarra alikuwa bado anaitumikia klabu ya kwao Salitas FC ya Burkina Faso, hatua ambayo ilifanya safari yake ya soka barani Afrika ianze kuchukua mwelekeo mpya. Licha ya uwezo wake kuonekana wazi, mambo hayakwenda kama ilivyotarajiwa upande wa Simba, na jina lake likabaki kuwa moja ya vipaji vilivyopita bila kusajiliwa rasmi.
Hatimaye, Esperance*waliinusa fursa hiyo na hawakusita kuichangamkia. Kwa kumchukua Diarra, ni wazi kabisa kwamba klabu hiyo ya Tunisia imeokota dodo la maana, mchezaji mwenye uwezo mkubwa ambaye sasa anathibitisha thamani yake uwanjani. Hii inabaki kuwa funzo kwa klabu zetu kuhusu umuhimu wa kufanya maamuzi ya haraka na sahihi pindi kipaji kinapojitokeza.
