Fiston Mayele Mfungaji Bora Ligi ya Mabingwa CAF 2025
Mwamba Fiston Mayele anapata kiatu cha pili cha ufungaji Bora kwenye michuano ya CAF
Kiatu chake cha kwanza alikipata akiwa na Yanga SC ya Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) akimaliza na magoli saba msimu wa 2023
Lakini mwaka huu 2025 Fiston Mayele ametwaa kiatu cha ufungaji Bora wa ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) akiwa na Pyramids FC akimaliza michuano hiyo na magoli 6 huku akitwaa Ubingwa wa CAF kwa mara ya kwanza