Edo Kumwembe na Jemedari Said Wararuana Kisa CAF Kukataa Uwanja wa Mkapa

jemedari said na Edo Kumwembe
jemedari said na Edo Kumwembe

Edo Kumwembe na Jemedari Said Wararuana Kisa CAF Kukataa Uwanja wa Mkapa

Sakata la mechi ya kombe la Shirikisho Afrika kati ya Simba Sc dhidi ya RS Berkane kuchezwa Zanzibar badala ya Benjamin Mkapa Dar es Salaam limeendelea kuwa kizungumkuti huku wachambuzi wakicharurana kwenye mijadala na hoja kuhusu maamuzi hayo ya CAF.

Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii Mchambuzi nguli Jemedari Said ameandika:

“KWA-MKAPA HATOKI MTU -Hii slogan iliyoanzishwa na Simba SC ndiyo hasa inawaumiza kichwa CAF, RS BERKANE na VIBARAKA wao.

Wanahofia kombe litabakia Tanzania, kama hali hii ya kiwanja ipo hivi leo, WHY mechi isichezwe ikachezwe Zanzibar? CAF waliwapa mashabiki wa Simba SC tunzo ya mashabiki bora Afrika wakiwa hata hawajacheza Nusu Fainali, lakini ile turn out yao kila game na namna wanavyohanikiza ushindi ilikuwa balaa, leo timu ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa.CAF ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ya CAF inatafuta ahueni ikacheze Zenji kwenye mashabiki 15,000 wanaogopa mashabiki 60,000/ watashusha gharika.

Nafahamu jitihada kubwa zilizofanywa na zinazoendelea kufanywa na Serikali, TFF na Simba SC juu ya kutumia uwanja wa Mkapa., nafahamu namna msimamizi/mkaguzi wa Viwanja wa CAF wa mwanza (Moustafa) ambaye alikuwa Mmorocco alivyokuwa anataka mechi ikachezwe Zanzbar akiogopa Kwa-Mkapa, nafahamu aliyeletwa pia anatoka Morocco.

Hapa kuna vita ya Morocco Vs Tanzania , kama una kichwa maji pekee ndio huwezi kujua hii kitu. Ila Morocco mpaka sasa wanasaidiwa na CAF kitu ambacho ni hatari sana.”

Hata hivyo mchambuzi mkongwe, Edo Kumwembe amejibu ‘posti’ hiyo ya Bin Kazumari kwa kuandika:

“Tumefungua uwanja mwaka 2007…mpaka leo mvua ikinyesha unatuama maji. Pambano la Simba na Al Masry liliharibika kwa sababu ya pitch kujaa maji.

Tangu hapo hakuna mechi ya CAF iliyochezwa hapo. Wachina wametupiga tunasingizia Wamorocco wanatuogopa. Moja kati ya sifa kubwa ya uwanja wetu katika mafaili yao ni hiyo. Akina Morisson washapiga sana chenga katika madimbwi.

Ebu tunyooke kidogo na kuwanyoosha wahusika. Mvua kali sio sababu ya uwanja kutuama maji. Tusipige siasa nyingine.”

ALSO READ | Viingilio Simba vs RS Berkane 25 May 2025

Leave a Comment

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *