Edo Kumwembe “Aziz K Ana Kauvivu Fulani Hivi Nilijua Kwa Waarabu Asingeweza”
Edo Kumwembe ✍️..”Hapa kwetu ilikuwa rahisi kwake kwa sababu leo Yanga wangecheza na Namungo na kumiliki mpira kwa asilimia 99. Keshokutwa wangecheza na Coastal na kumiliki mpira wote. Kule Morocco licha ya Wydad kuwa wakubwa, lakini mpira wao dhidi ya wapinzani ni kuhenya kwa dakika zote Aziz ana ‘kauvivu’ Fulani ambako nilijua Asingemudu sana mpira wa Waarabu wa kule.
Huku kwetu alitusisimua katika matukio ya mashuti. Kona nzuri. Faulo nzuri. Mashuti ya mbali. Pasi za mwisho katika eneo la mwisho ambalo Yanga mara zote walifika kwa urahisi.”
