Edo KumwembeEdo Kumwembe

Edo Kumwembe: Azam Waache Utani, Wajifunze Kwa Pyramids ya Mayele

Ubingwa wa Pyramids pia umenikumbusha kwamba suala sio umri wa klabu. Suala ni uwekezaji tu. Kigingi kikubwa kwao ni ubingwa wa Ligi Kuu Misri. Pale wamekutana na fitina za Al Ahly na mara nyingi wamejikuta wakiishia nafasi ya pili.
.
Hapa nimewakumbuka ndugu zetu Azam. Na wao walianza 2008 kama Pyramids. Tofauti ni kwamba Azam wamewahi kuchukua mara moja ubingwa wa Ligi Kuu wakati Pyramids hawajawahi. Mara nyingi Azam wamekuwa wakilalamika kwamba wakubwa wamekuwa wakiwapiga fitna katika mbio za ubingwa.
.
Sawa, kama unapigwa vita ndani basi unaweza kufanya kitu nje. Hiki ndicho ambacho rafiki zetu Pyramids wamewafundisha Azam. Kama marefa wa ndani wanazipendelea Simba na Yanga basi unaweza kuchezeshwa na waamuzi wa kimataifa katika mechi za CAF na ukachukua ubingwa kama una timu imara.
.
Azam wangeweza kukwepa fitna za Simba na Yanga kwa kufanya vizuri michuano ya CAF. Ingethibitisha namna gani huwa wananyongwa katika soka la nyumbani.
.
Kwa hali ilivyo sasa ni ngumu kuthibitisha kwa sababu katika michuano ya kimataifa nako wanavurunda. Majuzi tu walitolewa na timu ambayo haina hata afya kutoka Ethiopia. Wakatolewa tena na APR ya Rwanda. Maisha ambayo Simba na Yanga wameshavuka.”

— Legend, Edo Kumwembe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *