January 9, 2026

Dirisha Dogo Usajili Kwa Timu za Ligi Kuu Lafunguliwa Tanzania

0
20251226085024_-862158150_2422178188332356127_640_640_85_webp.webp

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania limetangaza kufunguliwa rasmi kwa dirisha dogo la usajili kwa klabu zinazoshiriki Ligi Kuu ya NBC (NBCPL), NBC Championship League (NBCCL), First League (FL) pamoja na Ligi Kuu ya Wanawake (TWPL) kwa msimu wa 2025/2026.

Dirisha hilo limefunguliwa leo Alhamis, Januari 1, 2026, na linatarajiwa kufungwa Januari 30, 2026. Klabu zote zinatakiwa kufanya usajili na uhamisho wa wachezaji kupitia mfumo wa FIFA Connect kama ilivyoelekezwa na shirikisho.

TFF imeeleza kuwa hakutakuwa na muda wa nyongeza baada ya tarehe ya mwisho ya usajili, hivyo klabu zinahimizwa kukamilisha taratibu zao kwa wakati ili kuepuka usumbufu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *